WeBible
Swahili
Select Version
Cherokee New Testament (1860) with Sequoyah transliterated forms
Sahidic NT
Czech BKR
1757 Church Slavonic Elizabeth Bible
Danish
Danish New Testament from 1819 with original orthography
Danish OT1871 + NT1907 with original orthography
Elberfelder (1871)
Elberfelder (1905)
Luther (1545)
Greek Modern
American Standard Version
Basic English Bible
Douay Rheims
William Tyndale Bible (1525/1530)
Webster's Bible
World English Bible
Weymouth NT
Young's Literal Translation
Esperanto
Reina Valera NT (1858)
Sagradas Escrituras (1569)
(Navarro Labourdin) NT
Finnish Bible (1776)
Pyha Raamattu (1933 1938)
Darby
Martin (1744)
Scots Gaelic (Gospel of Mark)
Gothic (Nehemiah NT Portions)
NT Tischendorf 8th Ed
Manx Gaelic (Esther Jonah 4 Gospels)
Aleppo Codex
OT Westminster Leningrad Codex
Croatian
Hungarian Karoli
Eastern (Genesis Exodus Gospels)
Western NT
Giovanni Diodati Bible (1649)
Riveduta Bible (1927)
明治元訳「舊約聖書」(1953年版) 大正改訳「新約聖書
Japanese Denmo 電網聖書
Japanese Kougo-yaku 口語訳「聖書」(1954/1955年版)
Japanese Raguet-yaku ラゲ訳「我主イエズスキリストの新約聖書」(1910年版)
Korean
Vulgata Clementina
Baiboly Malagasy (1865)
Sathyavedapusthakam (Malayalam Bible) published in 1910
Judson (1835)
Det Norsk Bibelselskap (1930)
Petrus Canisius Translation
Dutch Staten Vertaling
De ganse Heilige Schrift bevattende al de kanonieke boeken van het Oude en Nieuwe Testament, met de apocriefe (deuterocanonieke) boeken
Studentmållagsbibelen frå 1921
Polish Biblia Gdanska (1881)
Old Public Domain Pohnpeian Bible
Potawatomi (Matthew Acts) (Lykins 1844)
El Evangelio segun S. Lucas, traducido al Romaní, ó dialecto de los Gitanos de España
Synodal Translation (1876)
Albanian Bible
Serbian Bible Daničić-Karadžić Ekavski
Serbian Bible Daničić-Karadžić Ijekavski
Swedish (1917)
Svenska Karl XII:s Bibel (1703)
Svenska Karl XII:s Bibel (1873)
Swahili
Peshitta NT
Ang Dating Biblia (1905)
Klingon Language Version of the World English Bible
NT (P Kulish 1871)
Українська Біблія. Переклад Івана Огієнка.
Vietnamese (1934)
聖經 (文理和合)
Union Simplified
Union Traditional
Widget
Switch to light / dark version
swahili
Matendo 8
Matendo 8
8 / 28
1
Saulo naye alikiona kitendo hicho cha kumwua Stefano kuwa sawa. Siku hiyo kanisa la Yerusalemu lilianza kuteswa vibaya. Waumini wote, isipokuwa tu wale mitume, walilazimika kutawanyika katika sehemu za mashambani za Yudea na Samaria.
2
Watu wamchao Mungu, walimzika Stefano na kumfanyia maombolezo makubwa.
3
Wakati huohuo, Saulo alijaribu kuliangamiza kanisa. Alikwenda katika kila nyumba, akawatoa nje waumini, wanaume kwa wanawake, akawatia gerezani.
4
Wale waumini waliotawanyika, walikwenda kila mahali wakihubiri ule ujumbe.
5
Naye Filipo aliingia katika mji wa Samaria na kumhubiri Kristo kwa wenyeji wa hapo.
6
Watu walijiunga kusikiliza kwa makini ule ujumbe wa Filipo na kuona ile miujiza aliyoifanya.
7
Maana pepo wachafu waliokuwa wamewapagaa watu wengi waliwatoka wakipiga kelele kubwa; na pia watu wengi waliokuwa wamepooza viungo na waliolemaa waliponywa.
8
Kukawa na furaha kubwa katika mji ule.
9
Basi, kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Simoni ambaye alikuwa amekwisha fanya uchawi wake katika mji huo kwa muda na kuwashangaza watu wa Samaria, akijiona kuwa yeye ni mtu maarufu.
10
Watu wote, wadogo na wakubwa, walimsikiliza kwa makini wakisema, "Simoni ndiye ile nguvu ya kimungu inayoitwa <FO>Nguvu Kubwa."<Fo>
11
Walivutiwa sana naye kwa vile alikuwa amewashangaza kwa uchawi wake kwa muda mrefu.
12
Lakini walipouamini ujumbe wa Filipo juu ya Habari Njema ya Ufalme wa Mungu na jina la Yesu Kristo, walibatizwa, wanawake na wanaume.
13
Hata Simoni aliamini; baada ya kubatizwa ilikuwa akiandamana na Filipo, akastaajabia maajabu na miujiza iliyokuwa inafanyika.
14
Wale mitume waliokuwa kule Yerusalemu walipopata habari kwamba wenyeji wa Samaria nao wamelipokea neno la Mungu, waliwatuma kwao Petro na Yohane.
15
Walipofika waliwaombea hao waumini ili wampokee Roho Mtakatifu;
16
maana wakati huo Roho Mtakatifu hakuwa ameshukia yeyote kati yao; walikuwa wamebatizwa tu kwa jina la Bwana Yesu.
17
Basi, Petro na Yohane wakawawekea mikono hao waumini, nao wakampokea Roho Mtakatifu.
18
Hapo Simoni aling'amua kwamba kwa kuwekewa mikono ya mitume waumini walipewa Roho Mtakatifu. Hivyo aliwapa Petro na Yohane fedha akisema,
19
"Nipeni na mimi uwezo huo ili yeyote nitakayemwekea mikono, apokee Roho Mtakatifu."
20
Lakini Petro akamjibu, "Potelea mbali na fedha zako kwa vile unafikiri kwamba unaweza kununua karama ya Mungu kwa fedha!
21
Huna sehemu yoyote wala haki katika kazi hiyo kwa maana moyo wako hauko sawa mbele ya macho ya Mungu.
22
Kwa hiyo, tubu ubaya wako huu na umwombe Bwana naye anaweza kukusamehe fikira kama hizo.
23
Ni dhahiri kwangu kwamba umejaa wivu mkali na mfungwa wa dhambi!"
24
Simoni akajibu, "Tafadhali, niombeeni kwa Bwana lisije likanipata lolote kati ya hayo mliyosema."
25
Baada ya Petro na Yohane kutoa ushuhuda wao na kuutangaza ujumbe wa Bwana, walirudi Yerusalemu. Walipokuwa wanarudi walihubiri Habari Njema katika vijiji vingi vya Samaria.
26
Malaika wa Bwana alimwambia Filipo, "Jitayarishe uende kusini kupitia njia inayotoka Yerusalemu kwenda Gaza." (Njia hiyo hupita jangwani.)
27
Basi, Filipo akajiweka tayari, akaanza safari. Wakati huohuo kulikuwa na Mwethiopia mmoja, towashi, ambaye alikuwa anasafiri kuelekea nyumbani. Huyo mtu alikuwa ofisa maarufu wa hazina ya Kandake, malkia wa Ethiopia. Alikuwa amekwenda huko Yerusalemu kuabudu na wakati huo alikuwa anarudi akiwa amepanda gari la kukokotwa.
28
Alipokuwa anasafiri, alikuwa akijisomea kitabu cha nabii Isaya.
29
Basi, Roho Mtakatifu akamwambia Filipo, "Nenda karibu na gari hilo ukafuatane nalo."
30
Filipo akakimbilia karibu na gari, akamsikia huyo mtu akisoma katika kitabu cha nabii Isaya. Hapo Filipo akamwuliza, "Je, unaelewa hayo unayosoma?"
31
Huyo mtu akamjibu, "Ninawezaje kuelewa bila mtu kunielewesha?" Hapo akamwalika Filipo apande juu, aketi pamoja naye.
32
Basi, sehemu ya Maandiko Matakatifu aliyokuwa anasoma ilikuwa hii: "Alikuwa kama kondoo anayepelekwa kuchinjwa; kimya kama vile mwana kondoo anaponyolewa manyoya, yeye naye hakutoa sauti hata kidogo.
33
Alifedheheshwa na kunyimwa haki. Hakuna atakayeweza kuongea juu ya kizazi chake, kwa maana maisha yake yameondolewa duniani."
34
Huyo Mwethiopia akamwambia Filipo, "Niambie, huyu nabii anasema juu ya nani? Anasema mambo haya juu yake yeye mwenyewe au juu ya mtu mwingine?"
35
Basi, Filipo akianzia na sehemu hiyo ya Maandiko Matakatifu, akamweleza Habari Njema juu ya Yesu.
36
Walipokuwa bado wanaendelea na safari walifika mahali penye maji na huyo ofisa akasema, "Mahali hapa pana maji; je, kuna chochote cha kunizuia nisibatizwe?"
37
<FI> Filipo akasema, "Kama unaamini kwa moyo wako wote unaweza kubatizwa." Naye akajibu, "Naam, ninaamini kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu."<Fi>
38
Basi, huyo ofisa akaamuru lile gari lisimame; na wote wawili, Filipo na huyo ofisa wakashuka majini, naye Filipo akambatiza.
39
Walipotoka majini Roho wa Bwana akamfanya Filipo atoweke. Na huyo Mwethiopia hakumwona tena; lakini akaendelea na safari yake akiwa amejaa furaha.
40
Filipo akajikuta yuko Azoto, akapita katika miji yote akihubiri Habari Njema mpaka alipofika Kaisarea.
Copy Link
Webible
Freely accessible Bible
48 Languages, 74 Versions, 3963 Books
Widget